BURUDANI NA MICHEZO

Arsenal wabwagwa na Man City 6-3

 

Manchester City, wametoa ujumbe mkali kwa mahasimu wao kwenye ligi ya Premier Arsenal baada ya kuwacharaza mabao sita kwa matatu.

Upande wa Manuel Pellegrini uliwacharaza Arsenal na kuziba pengo la pointi tatu.Arsenal walilalamika wakitaka kupewa penalty moja ingawa kwa kweli Man City walikuwa wamejiandaa vilivyo dhidi ya Arsenal, huu ulikuwa kama upepo kwao.
Man City sasa wameingiza mabao 35 nyumbani katika mechi 58 katika uwanja wa Etihad.
Msimu huu City hawacharazi tu timu nyumbani bali wanang’oa pembe zao na ikiwa wanaweza kuonyesha mchezo kama huu hata wanapocheza ugenini bila shaka watakuwa katika msitari wa mbele kushinda kombe la ligi ya Premier.
Bao la Sergio Aguero lilifuatiwa na bao laTheo Walcott aliyecheka na wavu, lakini Alvaro Negredo akaiwezesha City kusalia mbele kabla ya kipindi cha kwanza cha mchezo.
Fernandinho aliiweka City mbele wakati wote ingawa Walcot aliingiza bao lengine la pili kabla ya City kuanza kushambulia Arsenal kutoka pande zote hasa baada ya David Silva Fernandinho tena kuingiza bao lengine kabla ya Per Mertesacker kuyanfa mabao 5-3 kabla ya mechi kumalizika.
City walifikisha mabao yao kuwa sita kufuatia penalti ya Yaya Toure kabla ya mechi kumalizika.



Mourinho:Chelsea mambo shwari sasa

Golkipa wa Chelsea, Petr Cech, aliokoa mabao kadhaa katika kipindi cha pili cha mechi kati ya Chelsea na Crystal Palace na kusalia na pointi mbili tu kufikia Arsenal wanaoongoza orodha kwa pointi.
Fernando Torres aliiweka Blues mbele katika uwanja wa Stamford Bridge baada ya shuti la Willian kugonga lango la bao na kuwakosesha bao lengine.
Crystal Palace hata hivyo walisawazisha kupitia kwa mchezaji, Marouane Chamakh kabla ya Ramires kuiweka Chelsea kifua mbele kwa mabao mawili kwa moja.
Mlinda lango, Cech aliwakosesha mabao Jason Puncheon, Damien Delaney na hatimaye Stuart O'Keefe huku wenyeji wakishinda kwa leo.
Wenyeji walifanikiwa kushinda kutokana na mabao yao ya dakika za mwisho 2-1.
Meneja wa klabu Jose Mourinho alisema kuwa Chelsea walikuwa matatani hasa baada ya kushindwa na Stoke wikendi iliyopita. Lakini sasa mambo shwari.


 

Manchester City yailima Arsenal


 Manchester City na Arsenal
Manchester City imetoa ujumbe muhimu kwa wapinzani wao kwa kuinyuka Arsenal
Mechi hiyo ilikuwa ya kusisimua kutokana na wingi wa magoli yaliyoingia,jumla ya magoli 9.Manchester City ilimaliza kipindi cha kwanza ikiongoza kwa 2-1 kutokana na magoli yaliyofungwa na Aguero na Negredo.
Kwa kile kilichoonekana kupwaya kwa ngome za timu mbili,Manchester City iliongezea magoli zaidi katika kipindi cha pili kwa kuwatumia Fernandinho aliyefunga magoli 2,Silva na Yaya Toure aliyefunga goli la mwisho kwa njia ya penalty.
Upande wa Arsenal Theo Walcott alipachika mabao 2 na mlinzi Mertesacker akafunga goli la 3.
Ushindi huo wa Manchester City unawasaidia kupunguza pengo la alama tatu lililokuwepo kati ya timu mbili na kuonya Arsenal kuwa bado ina kazi ya kufanya licha ya kwendelea kuongoza ligi ikiwa na alama 35.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni