Jumatano, 9 Julai 2014

SIMBA SC WAANZA KUJIFUA KESHO BOKO


KIKOSI cha Simba ya jijini Dar es Salaam kinatarajia kuanza mazoezi kesho kwenye Uwanja wa Boko Veteran ulioko Boko kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara imeelezwa. Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo mjini Dar es Salaam, Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola, amesema kuwa tayari wachezaji wa timu hiyo wameshapewa taarifa za kuanza kwa mazoezi hayo tayari kunoa makali kwa msimu mpya wa ligi. Matola amesema kuwa mazoezi yataanzia gym Chang'ombe na jioni yatakuwa uwanjani.
Suleiman Matola kulia akiwa na bosi wake, Zdravko Logarusic 
Amesema kuwa licha ya kuchelewa kuanza maandalizi yake, wanaamini wachezaji watakuwa kwenye kiwango cha juu kutokana na kila mmoja kufanya mazoezi binafsi. "Kabla mwalimu ( Zdravko Logarusic) hajaondoka, aliwaeleza wachezaji wajitunze na wawe wanafanya mazoezi ili kujiweka tayari na programu alizoziandaa za msimu mpya," amesema. Kikosi hiko kinatarajia kuanza mazoezi chini ya Matola, kutokana na Logarusic, kuchelewa kuwasili nchini kama ilivyotarajiwa. Habari za ndani zilizopatikana jana mchana zinasema kwamba Mcroatia huyo atawasili nchini Alhamisi na Ijumaa ataungana na wachezaji wake kuendelea na mazoezi. Simba pia inatarajia kuelekea Afrika Kusini kuweka kambi ya siku 17 na itaondoka nchini Julai 20. Hata hivyo katika kambi hiyo huenda ikawakosa nyota wake watano walioko katika timu ya Taifa (Taifa Stars) ambao wanajiandaa kuikabili Msumbiji. Nyota hao ni pamoja na Ramadhan Singano 'Messi', Amri Kiemba, Jonas Mkude, Joram Mgeveke na Haroun Chanongo.
ARUSHA: - Hali ya wasiwasi imeendelea kutanda katika Jiji la Arusha baada ya kitu kinachoaminika kuwa ni bomu kutegwa katika mkahawa mmoja jijini humo.

Walichofanywa Brazil na Ujerumani hiki hapa

20140709-014045-6045392.jpg
Michuano ya kombe la dunia leo imechukua sura nyingine kabisa baada ya mchezo wa kwanza wa nusu fainali kati ya wenyeji Brazil dhidi ya Ujerumani.
Kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Belo Horizonte – Ujerumani wameweka historia ya mbili kubwa – kutinga fainali ya 8 ya kombe la dunia – hii ni mara nyingi kuliko timu zote duniani, pili kuifunga Brazil nyumbani kwao ikiwa ni mara ya kwanza kwa Brazil kupoteza mechi ya ushindani kwenye ardhi yao tangu mwaka 1975.
Magoli ya Ujerumani yalifungwa na Muller, Toni Kroos mawili, Sami Khedira, Ander Schurrle nae akafunga mawili huku Oscar akiifungia Brazil goli moja la kufutia machozi katika mechi iliyoishwa kwa ushindi wa 7-1.
Ujerumani sasa anamsubiri mshindi wa kati ya Argentina vs Uholanzi hapo kesho ili kupata kujua mpinzani wake wa fainali itakayopigwa jumapili hii.

Disbelief: Fernandinho, Maicon and David Luiz look bemused following Germany's fifth goal of the evening
Lawama: Wachezaji wa Brazil, kutoka kushoto Fernandinho, Maicon na David Luiz 
Opener: Thomas Muller scores Germany's first to set Joachim Low's men on their way
La kwanza: Thomas Muller akiifungia Ujerumani bao la kwanza
Back of the net! Goalkeeper Julio Cesar is powerless to stop Thomas Muller's effort as David Luiz watches on
Kipa Julio Cesar akishindwa kuzuia shut la Thomas Muller, huku David Luiz akiangalia
Record-breaker: Miroslav Klose celebrates after becoming the top scorer in World Cup history
Mvunja rekodi: Miroslav Klose akishangilia baada ya kuibuka mfungaji bora wa kihistoria wa Kombe la Dunia
On his knees: Klose broke Brazil legend Ronaldo's goalscoring record as he doubled Germany's advantage
Klose amevunja rekodi ya gwiji wa Brazil, Ronaldo akifunga mabao mawili leo
Lethal finisher! Klose guides the ball into the net as Brazil midfielder Fernandinho watches on
Klose akifunga huku kiungo wa Fernandinho akimsindikiza kwa macho
Kroos-ing to victory: Kroos wheels away to celebrate after scoring his second goal two minutes after his first
Kroos akiondoka kushangilia baada ya kufunga
Easy does it: Sammy Khedira slots the ball home to give Germany into a 5-0 lead on 29 minutes
Sammy Khedira akiifungia Ujerumani bao la tano
Delight and despair: Germany celebrate while Brazil players look on inside the Estadio Mineirao
Ujerumani wakipongezana huku, wachezaji wa Brazil wakitawanyika Uwanja wa Mineirao
Fall to the floor: Brazil defender David Luiz is grounded under the challenge of Miroslav Klose
Beki wa Brazil, David Luiz akienda chini wakati anakabiliana na Miroslav Klose
Midfield battle: Germany's Sami Khedira races forward away from Brazil's Luis Gustavo
Sami Khedira akimtoka Luis Gustavo wa Brazil
Halted: Germany defender Mats Hummels stops striker Fred in his tracks as Oscar looks to retrieve the ball
Beki wa Ujerumani, Mats Hummels akimzuia Fred huku Oscar akiwa tayari kutoa msaada
Little and large: Germany defender Jerome Boateng towers over Brazil left back Marcelo
Beki wa Ujerumani, Jerome Boateng akizinguana na Marcelo wa Brazil

MAN UNITED WAANZA MAZOEZI, WA ‘MKOPO’ BEBE, ANDERSON, ZAHA….WAREJEA!


MAN-UNITED-TOUR2014-LOGO-BESTMANCHESTER UNITED Jana walianza Mazoezi rasmi kwa ajili ya Ziara ya Kabla Msimu Mpya ya huko Marekani na Wachezaji kadhaa waliokuwa nje kwa Mkopo Msimu uliopita wamerejea na kujumuika huko AON Training Complex Jijini Manchester
Kutokuwepo kwa Meneja mpya, Louis van Gaal, ambae bado yuko Brazil akiiongoza Netherlands kwenye Kombe la Dunia, kulikifanya Kikosi hicho kuwa chini ya Meneja Msaidizi Ryan Giggs.
Wachezaji hao walianza kurudi Klabuni tangu Ijumaa iliyokwisha kwa ajili ya upimwaji Afya zao na Mazoezi rasmi kupangwa kuanza Jana Jumatatu.
Miongoni mwa Wachezaji wa Timu ya Kwanza waliokuwepo hiyo Jana ni pamoja na Mchezaji mpya Ander Herrera na kina Jonny Evans, Michael Carrick, Darren Fletcher, Tom Cleverley na Rafael Da Silva.
Lakini pia Wachezaji kadhaa waliokuwa nje kwa Mkopo Msimu uliopita walirejea na hao ni kina Bebe, Anderson, ZAHA-MAN_UNITEDWilfried Zaha, Angelo Henriquez, Jesse Lingard na Nick Powell.ANDERSON
Bebe alikuwa huko kwao Ureno na Klabu ya Paços de Ferreira, Anderson alikuwa Italy na Fiorentina huku Angelo Henriquez, Mchezaji kutoka Chile, alichezea Real Zaragoza.
Msimu uliopita Wilfried Zaha alikuwa Cardiff City, Jesse Lingard alikuwepo Brighton na Nick Powell kuichezea Wigan Athletics.
Wiki hii, Ryan Giggs anatarajiwa kukutana na kila Mchezaji na kuongea nao ana kwa ana.
Wachezaji wengine ambao wamechelewa kujiunga wenzao ni wale waliokuwepo huko Brazil na Timu zao za Taifa kwenye Fainali za Kombe la Dunia lakini baadhi yao wanatarajiwa wote kuwepo kwenye Ziara ya Mareakani.
Hao ni pamoja na Shinji Kagawa, aliekuwa na Japan huko Brazil, David De Gea, aliekuwa na Spain na Wachezaji wa England ambao ni Wayne Rooney, Chris Smalling, Phil Jones, Danny Welbeck na Mchezaji mpya Luke Shaw.
Man United wataruka hapo Julai 18 kuelekea huko Marekani na kupiga Kambi huko California kabla ya kucheza Mechi yao ya Kwanza huko USA hapo Julai 23 dhidi ya LA Galaxy kugombea Chevrolet Cup ndani ya Rose Bowl, Pasadena.
USA-ZIARA YA KABLA MSIMU MPYA:
[Zote Nchini Marekani]
Manchester United v LA Galaxy
Chevrolet FC Cup
Jumatano 23 Julai 2014, Rose Bowl, Pasadena
Manchester United v AS Roma
International Champions Cup
Jumamosi 26 Julai 2014, Sports Authority Field, Denver
Manchester United v Inter Milan
International Champions Cup
Jumanne 29 Julai 2014, FedEx Field, Washington DC
Manchester United v Real Madrid
International Champions Cup
Jumamosi 2 Agosti 2014, Michigan Stadium, Ann Arbor

Jumamosi, 14 Desemba 2013

Hali tete baraza la mawaziri


Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete, imeanza kuwahoji mawaziri waliotajwa ni ‘mzigo’ kwa Serikali.
Hata hivyo, habari za ndani zilieleza kwamba miongoni mwa ajenda kuu za CC ni kuwahoji mawaziri wanaolalamikiwa na wananchi, kwamba wameshindwa kutekeleza majukumu yao.



Maelfu wakwama kumuaga Mandela

 
Maelfu ya wananchi wa Afrika Kusini wameshindwa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Rais wa Kwanza mzalendo wa nchi hiyo, Nelson Mandela kutokana na muda uliopangwa kumalizika.
Kuanzia Jumatano wiki hii hadi jana, mwili wa Mandela aliyefariki dunia Desemba 4 mwaka huu, ulikuwa ukiwekwa katika Ikulu ya Pretoria, iliyopo ndani ya Majengo ya Umoja (Union Buildings), kila asubuhi kwa ajili ya wananchi kutoa heshima za mwisho.
Jana ilikuwa siku ya mwisho ya utoaji wa heshima hizo na hadi muda uliowekwa ulipokwisha saa 11:30 jioni, kulikuwa na maelfu ya watu waliokosa fursa ya kumuaga mpendwa wao huyo.
Dalili za idadi kubwa ya watu kukosa nafasi hiyo adhimu zilianza kuonekana Jumatano na baadaye juzi Alhamisi kwani hadi muda wa kufunga ulipofika jioni, maelfu ya watu walirejea nyumbani bila kupata fursa ya kuaga.
Jana mchana, Serikali ilitoa taarifa kwamba kwa kuzingatia idadi ya watu waliojitokeza kutoa heshima zao za mwisho, ilikuwa vigumu kwa watu wote kufikiwa.




Lowassa anusurika ajali ya ndege Arusha



Abiria 37 waliokuwa wamesafaria ndege ya Shirika la Precision Air, akiwamo Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, jana walinusurika kifo, baada ya magurudumu manne ya ndege hiyo kupasuka ilipokuwa ikitua katika Uwanja wa Ndege wa Arusha.
Tukio hilo la aina yake, lilitokea saa 6:15 mchana, wakati ndege hiyo, ikitua kutoka jijini Dar es Saalam, ikiwa na abiria hao 37, marubani wawili na wahudumu wawili.
Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza hakuna majeruhi aliyeripotiwa.
“Hadi sasa hali ni shwari, ndege iliweza kusimama licha ya kupasuka magurudumu. Kiutaratibu uchunguzi umeanza kufanywa na wataalamu husika,”alisema Kamanda Sabas.

Ijumaa, 6 Desemba 2013

Mandela afariki dunia


RAIS wa kwanza wa Afrika Kusini na mpinga siasa za ubaguzi wa rangi, Nelson Mandela amefariki nchini humo akiwa na umri wa miaka 95.
Taarifa za kifo chake zimetangazwa na rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma ambaye amesema Mandela amefariki majira ya saa 2.50 usiku wa Alhamisi kwa saa za Afrika Kusini.
Mandela amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwenye mapafu kwa muda mrefu, alilazwa na baadaye kuruhusiwa kutoka hospitali ambapo mauti yamemkuta akiwa nyumbani kwake mjini Pretoria.
Tayari viongozi mbalimbali duaniani wameshaanza kutuma salamu za rambirambi kwa familia na taifa la Afrika Kusini.
Viongozi hao ni pamoja na Rais Barack Obama wa Marekani na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-Moon.

Alhamisi, 5 Desemba 2013

80 wauawa kwenye mapigano A.Kati


Baraza la Usalama la umoja wa mataifa limeidhinisha kutumwa maelfu ya majeshi ya Afrika na wa Ufaransa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.Hali imeendelea kuwa mbaya nchini humo huku mapigano yakichacha usiku kucha na leo mchama mzima. Takriban watu 80 wameripotiwa kuuawa kwenye mapigano makali mjini Bangui Alhamisi.
Mji huo ulivamiwa na wafuasi wa Francois Bozize aliyeng'olewa mamlakani na waasi mwezi Machi hali iliyotumbukiza nchi hiyo katika mgogoro wa kisiasa.
Mapigano makali ya kurushiana risasi na silaha nzito nzito yalishuhudiwa mapema leo katika mji wa Bangui kabla Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la kupeleka majeshi ya kutoka Afrika na Ufaransa.
Mwandishi wa habari wa BBC aliyepo katika mji wa Bangui anasema aliona magari ya kivita yakiendeshwa kupita katika mitaa na kwamba watu wengi bado wamejifungia majumbani mwao.
Balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa Gerald Araud ameiambia BBC kuwa kuongezwa majeshi ya kimataifa utasaidia hali ya usalama ndani ya wiki chache.
Bwana Araud amesema Majeshi ya Umoja wa Afrika na yale ya Umoja wa Mataifa yanapaswa kusimamia sheria na utulivu katika mji wa Bangui kabla ya kuangalia usalama katika miji mingine nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati.




Lissu: Muswada wa kura za maoni ni kinyume cha Katiba

  
Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni imetaka Muswada wa Kura ya Maoni uondolewe bungeni hadi hapo Bunge litakapofanya marekebisho ya Katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa unapingana nayo.
Awali, muswada huo ulikuwa ujadiliwe katika Mkutano wa 12 wa Bunge lakini uliahirishwa kutokana na wajumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ya Bunge wanaotoka Zanzibar kupinga vikali kura ya maoni kupigwa visiwani humo kwa kuwa tayari huko kuna sheria hiyo.Akiwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni jana, Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, Tundu Lissu alisema katika Katiba ya sasa, hakuna mahali ambako kura ya maoni inatajwa.



JK asafisha vyombo vya dola Z’bar



Katika kile kinachotafsiriwa kuwa ni kusafisha idara zilizopo ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Rais Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko katika Idara ya Uhamiaji baada ya kumteua Johari Masoud Sururu kuwa Kamishna mpya wa Zanzibar.
Uteuzi huo wa Rais Kikwete umekuja siku moja tangu alipomteua Kamishna wa Polisi, Hamdan Omari Makame kushika wadhifa huo Zanzibar huku aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo, Kamishna Mussa Ali Mussa akiteuliwa kushika wadhifa mpya wa Kamishna wa Polisi Jamii.
Taarifa iliyotolewa jana na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga ilieleza kuwa kutokana na uteuzi huo, aliyekuwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Mwinchumu Hassan Salim atapangiwa kazi nyingine. Kabla ya uteuzi huo ambao umeanza Novemba 24 mwaka huu, Sururu alikuwa Mwambata wa Uhamiaji katika Ubalozi wa Tanzania, Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Jumatano, 4 Desemba 2013

Mamia ya wanahabari nchini Kenya wameandamana nchini humo kupinga sheria mpya ya vyombo vya habari iliyopendekezwa na wabunge na kufanyiwa mageuzi na Rais Uhuru Kenyatta.


Wanahabari hao waliokisiwa kuwa 300 baadhi wakiwa wameziba midomo yao kwa karatasi ya gundi (masking tape) kama ishara ya kukandamizwa, waliwasilisha malalamiko yao kwa bunge la taifa.
Sheria hiyo ambayo bado ni rasimu, itajadiliwa bungeni baada ya Rais kuikataa ilivyoandikwa akiwataka wabunge kuifanyia mabadiliko kabla ya kuifanya sheria.
Wakosoaji wanasema sheria hiyo ikiwa itapitishwa itabana uhuru wa vyombo vya habari licha ya mageuzi yaliyopendekezwa na Rais mwenyewe.
Wanadai kuwa mapendekezo hayo mapya ni makali zaidi kwa uhuru wa vyombo vya habari hata kuliko mapendekezo ya hapo awali yaliyoidhinishwa na bunge kabla ya bwana Kenyatta kukataa kutia saini.

Lissu: Mabadiliko makubwa yanakuja upinzani bungeni

 
Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni, itafanya mabadiliko makubwa katika Baraza lake Kivuli wakati wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Bunge unaoanza leo mjini Dodoma.
Panga pangua hiyo ambayo imesukumwa na kuvuliwa nyadhifa zote kwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe itawalenga pia mawaziri vivuli walioshindwa kutimiza majukumu yao kikamilifu.
Habari zilizopatikana jana mjini Dodoma zilisema Zitto ni mlengwa mkuu wa mabadiliko hayo ikiwa ni utekelezaji wa maazimio ya Kamati Kuu (CC) ya chama chake.