Alhamisi, 5 Desemba 2013

80 wauawa kwenye mapigano A.Kati


Baraza la Usalama la umoja wa mataifa limeidhinisha kutumwa maelfu ya majeshi ya Afrika na wa Ufaransa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.Hali imeendelea kuwa mbaya nchini humo huku mapigano yakichacha usiku kucha na leo mchama mzima. Takriban watu 80 wameripotiwa kuuawa kwenye mapigano makali mjini Bangui Alhamisi.
Mji huo ulivamiwa na wafuasi wa Francois Bozize aliyeng'olewa mamlakani na waasi mwezi Machi hali iliyotumbukiza nchi hiyo katika mgogoro wa kisiasa.
Mapigano makali ya kurushiana risasi na silaha nzito nzito yalishuhudiwa mapema leo katika mji wa Bangui kabla Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la kupeleka majeshi ya kutoka Afrika na Ufaransa.
Mwandishi wa habari wa BBC aliyepo katika mji wa Bangui anasema aliona magari ya kivita yakiendeshwa kupita katika mitaa na kwamba watu wengi bado wamejifungia majumbani mwao.
Balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa Gerald Araud ameiambia BBC kuwa kuongezwa majeshi ya kimataifa utasaidia hali ya usalama ndani ya wiki chache.
Bwana Araud amesema Majeshi ya Umoja wa Afrika na yale ya Umoja wa Mataifa yanapaswa kusimamia sheria na utulivu katika mji wa Bangui kabla ya kuangalia usalama katika miji mingine nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati.




Lissu: Muswada wa kura za maoni ni kinyume cha Katiba

  
Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni imetaka Muswada wa Kura ya Maoni uondolewe bungeni hadi hapo Bunge litakapofanya marekebisho ya Katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa unapingana nayo.
Awali, muswada huo ulikuwa ujadiliwe katika Mkutano wa 12 wa Bunge lakini uliahirishwa kutokana na wajumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ya Bunge wanaotoka Zanzibar kupinga vikali kura ya maoni kupigwa visiwani humo kwa kuwa tayari huko kuna sheria hiyo.Akiwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni jana, Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, Tundu Lissu alisema katika Katiba ya sasa, hakuna mahali ambako kura ya maoni inatajwa.



JK asafisha vyombo vya dola Z’bar



Katika kile kinachotafsiriwa kuwa ni kusafisha idara zilizopo ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Rais Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko katika Idara ya Uhamiaji baada ya kumteua Johari Masoud Sururu kuwa Kamishna mpya wa Zanzibar.
Uteuzi huo wa Rais Kikwete umekuja siku moja tangu alipomteua Kamishna wa Polisi, Hamdan Omari Makame kushika wadhifa huo Zanzibar huku aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo, Kamishna Mussa Ali Mussa akiteuliwa kushika wadhifa mpya wa Kamishna wa Polisi Jamii.
Taarifa iliyotolewa jana na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga ilieleza kuwa kutokana na uteuzi huo, aliyekuwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Mwinchumu Hassan Salim atapangiwa kazi nyingine. Kabla ya uteuzi huo ambao umeanza Novemba 24 mwaka huu, Sururu alikuwa Mwambata wa Uhamiaji katika Ubalozi wa Tanzania, Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni