Jumamosi, 10 Agosti 2013

Je Tsvangirai alijichimbia kaburi lake?

Minong'ono ilikithiri kwa miaka mingi. Wengi wakasema sio mjanja . Anapenda kucheza Golf sana . Ndio ni jasiri kwa uhakika , lakini mtu asiye na mikakati.
Huyu ndiye mwanasiasa aliyejaribu mara tatu kuwa rais wa Zimbabwe lakini hakuwahi kufua dafu hata siuku moja.
Morgan Tsvangirai, sasa anatupia macho hali ya kusahaulika kisiasa kufuatia chama chake kushindwa vibaya katika uchaguzi mkuu uliokamilika wiki jana, na kuna watu wengi wanahisi kuwa alipaswa kushindwa.
Hata ikiwa madai anayoyatoa kuwa kura ziliibwa na chama tawala ZANU-PF yatathibitishwa na majirani wa Zimbabwe wakitaka uchaguzi kurejelewa, rais Robert Mugabe hajaona sababu kubwa ya kuhofia upinzani mkubwa kwa utawala wake.

Sasa kwa nini Tsvangirai alaumiwe?

Wadadisi wanasema kosa kubwa ambalo yeye na chama cha MDC walifanya, ni uamuzi wake wa kujiondoa kutoka kinyang'anyiro cha mwaka 2008 kwa sababu ya ghasia zilizotokea baada ya utata uliofuata uchaguzi huo na kujiunga na rais Mugabe katika serikali ya Muungano.
Na kama wanavyosema , Tsvangirai alimuwezesha mpinzani wake kushikilia wadhifa wakati yeye mwenyewe hakuwa na ushawishi mkubwa.
Hatua ya Tsvangirai ilizua utata mkubwa na kupingwa na washirika wake wa karibu wa MDC - ingawa kunao wanaosema kuwa hatua yake ilikuwa sawa.
Wafuasi wa Mugabe wakisherehekea ushindi wake wiki jana
Zimbabwe ilikuwa katika hali ngumu - uchumi ulikuwa unaporomoka.
Kwa kujiunga na serikali ya Muungano, Tsvangirai alionekana kutojali maslahi ya wafuasi wake wakati yake akiyapa kipaombele.
Hata hivyo kosa kubwa ambalo Tsvangirai alifanya ni kutojitetea wakati akiwa katika serikali ya Muungano na Mugabe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni