Mwanamke maarufu zaidi duniani Oprah Winfrey amekumbana ana kwa ana
na kile anachokiita kitendo cha Ubaguzi wa rangi nchini Switzerland
baada ya muuza duka mmoja kukataa kumuuzia mkoba wa kike wa mkononi na
kumwambia kuwa hangeweza gharama yake.
Oprah ambaye ametajwa katika vitabu vya Forbes
kama mwanamke mwenye ushawishi mkubwa wa kisiasa duniani na mmoja wa
watu tajiri zaidi amedai kuwa msichana aliyekuwa akiuza hapo dukani
alimdharau kutokana na rangi yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni