Umoja wa Mataifa umesema ndege zake za kijeshi
zilizoko Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zimefanya
mashambulio dhidi ya waasi wa M-23 viungani mwa mji wa Goma.
Waasi wa M23 waliuteka na kuuthibiti mji huo wa Goma kwa muda mwaka uliopita na mapigano ya hivi karibuni yameongeza wasi wasi kuwa huenda waasi hao wakaishambulia tena mji huo.
Kikosi hicho maalum cha Umoja wa Mataifa kimepewa idhini ya kufanya mashambulio dhidi ya waasi ikiwa kutatokea haja ya kufanya hivyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni