Ijumaa, 22 Novemba 2013

Bara yataja silaha zake Chalenji

Michuano ya Chalenji itafanyika nchini Kenya kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 12 mwaka huu
Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 watakaoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji.
Michuano ya Chalenji itafanyika nchini Kenya kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 12 mwaka huu.
Kikosi kamili cha Kilimanjaro Stars kinaundwa na makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Gor Mahia,Kenya) na Aishi Manula (Azam).
Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting) na Said Moradi (Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Ramadhan Singano (Simba) na Salum Abubakar (Azam).
Washambuliaji ni Elias Maguli (Ruvu Shooting), Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni