Jumamosi, 23 Novemba 2013

Mtikisiko Chadema: Zitto awekwa benchi, Arfi ang'atuka, lawama zatanda

http://radiomoshifm.blogspot.com/p/blog-page.html

Mgogoro ndani ya Chadema umezidi kupamba moto baada ya Kamati Kuu kuwavua uongozi Zitto Kabwe na Dk Kitila Mkumbo, huku Makamu Mwenyekiti Taifa, Said Arfi akiandika barua ya kujiuzulu.


Zitto alivuliwa uongozi wa Naibu Katibu Mkuu Taifa na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, wakati Dk Mkumbo amevuliwa ujumbe wa Kamati Kuu. Wawili hao wanatuhumiwa kukisaliti chama.
Taarifa zilisema hoja ya kukisaliti chama pia ilimkumba Arfi akidaiwa kumwezesha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kupita ubunge bila kupingwa, katika uchaguzi mkuu uliopita na ndiyo sababu ya kuamua kuachia ngazi nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Taifa.
Mbali ya kuwavua uongozi Zitto na Dk Mkumbo, pia Kamati Kuu imewapa siku 14 wajieleze kwa nini wasifukuzwe uanachama. Kwa uamuzi huo Zitto amebaki na wadhifa wa ubunge wake wa Kigoma Kaskazini na wadhifa mwingine kwenye Kamati ya Bunge.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni