Jumamosi, 23 Novemba 2013

Ngugi awashambulia wasomi barani Afrika


 
Nguli wa Fasihi za lugha za Kiafrika na mtunzi wa vitabu maarufu, Profesa Ngugi wa Thiong’o amewashukia wasomi na viongozi wa Kiafrika kwa kukosa uzalendo wa kuzitumia lugha zao na badala yake, kuzitukuza za kigeni.
Akihutubia katika Chuo Kikuu cha Dar es Saalam jana, kuhusu lugha za Kiafrika na Ulaya, aliwataja wasomi na viongozi wa Serikali kuwa ni majemadari wa Afrika walioshikwa mateka na adui wanaowalazimisha kufanya kila kitu wanachowaamuru.
Ngugi anayetarajiwa kutunukiwa shahada ya heshima na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo, alisema wasomi wa wakati wa uhuru wanatofautiana sana na wa sasa.
Alisema wasomi wa sasa wameacha misingi ya utamaduni wa Mwafrika na badala yake, wanatukuza wazungu.



 

Majambazi yateka nyara magari, yapora mali

Zaidi ya watu 10 wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wameteka magari na kuwanyang’anya mali zao abiria katika Kijiji cha Ngararambe, wilayani Biharamulo, mkoani Kagera.

Vitendo hivyo vimejitokeza katika matukio mawili tofauti.
Tukio la kwanza lilitokea saa 2:00 asubuhi baada ya majambazi kuteka Hiece iliyokuwa ikitokea katika Kijiji cha Nyakahula kwenda Kijiji cha Lusahunga katika mnada wa ng’ombe.
Tukio la pili lilitokea saa 9:00 alasiri katika Pori la Kitongoji cha Busili kilometa kadhaa kutoka Kijiji cha Ngararambe ambapo majambazi waliteka magari mawili.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe, alisema majambazi hao walikuwa na silaha za jadi na bunduki aina ya SMG.
“Tulikwenda katika eneo la tukio na tukapambana nao kwa dakika 10 hadi walipotokomea,” alisema Kamanda Mwaipajati.
Alisema katika shambulio hilo, dereva wa gari la abiria alijeruhiwa vibaya.

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni