Jumapili, 24 Novemba 2013

‘Nilikuwa naomba Mungu kila siku ili afukuzwe Chadema’ - Mama Zitto




 

Siku moja baada ya Kamati Kuu ya Chadema kumvua uongozi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Taifa wa chama hicho, Zitto Kabwe, mama yake mzazi, Shida Salum ametoa ya moyoni akieleza kuwa kilichomkuta mwanaye kimefunika mabaya mengi yaliyopangwa afanyiwe.
“Kwa upande wangu naona kama ni ushindi kwa Zitto kutokana na jinsi ninavyojua hali ilivyo, mambo yalikuwa ni mengi mno na nikwambie tu, Zitto kuvuliwa uongozi kumefunika hayo yaliyokuwa yamekusudiwa kufanywa dhidi yake. Nilikuwa naomba Mungu  kila siku ili afukuzwe Chadema,” alisema mama huyo wakati akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Tabata, Dar es Salaam.
Shida Salum alisema kuwa Mungu amemnusuru mwanaye na kusisitiza, “Watu walikaa na kutengeneza ripoti ya siri kuhusu Zitto na kuiweka kwenye mtandao kisha kuituma kwa wanachama wa Chadema wanaowafahamu. Mpaka wanafikia hatua hiyo maana yake ni kwamba wamejaribu njia zote za kummaliza, lakini wameshindwa.”
Alisema kutokana na hali ilivyo hivi sasa amemnyang’anya mwanaye kwa muda simu zake zote za mkononi, kompyuta mpakato (Laptop) pamoja na iPad ili asiwasiliane na watu, kwa maelezo kuwa wapo wenye nia mbaya wanaomsaka kumpa pole za kinafiki.




Laptop ilichangia mauaji ya kutisha Ilala Bungoni
 
  • Desemba mwaka jana ni wakati, Gabriel Munisi alipokutana na Christina Newa. Awali lilikuwa penzi, ambalo Christina aliamini litampa faraja na kuyabadili maisha yake.
  •  Hata hivyo, ndoto yake hiyo ilibadilika muda mfupi tu wa penzi hilo baada ya mpenzi wake, Munisi, kuanza kuonyesha ukali uliopitiliza, wivu na maneno makali.
  • “Gaby alikuwa anaishi kwa kasumba, hajiamini, mkorofi na aliyependa kunitishia kwa kutumia silaha mara kwa mara,” anasema Christina.
    Ukali wa Munisi haukupungua licha ya Christina kujaribu kumbadili hata kumshauri aonane na daktari wa masuala ya saikolojia ambaye anaweza kumtibu.
     “Nilimwona si wa kawaida. Nilipomshauri kuhusu tiba, alikubali na akampigia simu daktari mmoja aliyekuwa hospitali ya Bugando ambaye alikubali kuwa, inawezekana Gaby ana matatizo ya kisaikolojia na wakakubaliana kuwa ataanza tiba,” anasema.
    Christina baada ya kuona penzi lake na Munisi limekithiri kwa  misuguano, mifarakano na vitisho, alishauriana na familia yake, kisha wakaamua kuwa aende kusoma katika Visiwa vya Cypruss, ili kujiongezea maarifa lakini pia atakuwa mbali na Munisi ambaye alikuwa sasa anaonekana kuwa tishio. 
    Munisi alionekana kuwa tishio mara baada ya kumtakia hadharani Christina kuwa endapo atamchezea ataisambaratisha familia yake akianzia na Goba, anakoishi mama yao, Ellen Eliezer, kisha Zanzibar anakoishi mdogo wake, Alpha Newa na kumalizia Ilala, inakoishi familia hiyo.

     

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni