Jumatano, 27 Novemba 2013

Zitto ajiweka njia panda

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe amejiweka katika mazingira magumu zaidi kisiasa ndani ya chama hicho, kutokana na shaka kubwa iliyougubika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Dar es Salaam juzi.
Zitto pamoja na viongozi wengine wawili wa Chadema; Dk Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba walivuliwa nyadhifa zao na Kamati Kuu ya Chadema baada ya kubainika kupanga mbinu za uasi, kupitia waraka ambao ulikuwa ukieleza mkakati wa kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani.


Pinda azitaka Serikali za Mitaa kugawa maeneo ya uwekezajiWaziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema, Serikali za Mitaa zikiweza kujisimamia na kutoa maeneo kwa ajili ya uwekezaji, zinaweza kupiga hatua za kiuchumi.

Pia amezishauri  serikali hizo kuonyesha fursa zilizopo katika uwekezaji  kwa lengo la kuwashawishi wawekezaji.
Pinda aliyasema hayo jana wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa  Ushirikiano wa Serikali za Mitaa kati ya Tanzania na China.
Mkutano huo unawashirikisha wafanyabiashara kutoka China na Tanzania, magavana na mameya, makuu wa mikoa, wakurugenzi wa halmashauri za mikoa na wakuu wa wilaya.



Jaji Mkuu aagiza kesi ya Mramba, wenzake iharakishwe 

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman, ameagiza kesi ya matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia Serikali hasara ya Sh11.7bilioni inayowakabili mawaziri wawili wa zamani na katibu mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha, imalizwe haraka.

Mawaziri hao ni Basil Mramba na Daniel Yona na katibu Grey Mgonja, ambao kesi yao iko  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni