Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amesema tuhuma alizosomewa na uongozi wa Chadema katika kikao cha Kamati Kuu sizo zilizoelezwa na chama hicho mbele ya waandishi wa habari na viongozi wa chama hicho.
Aidha, amesema kuwa vita aliyopo siyo kati
ya Chadema na Zitto, bali ni vita ya watu wengi, akitaja magenge ya watu
wanaotaka urais 2015 na walioficha fedha nje ya nchi walioungana
wakiona tatizo lao ni yeye hivyo kutaka kumwondoa bungeni.

Vidonge vya Uzazi wa Mpango vyadaiwa kusababisha upofu
Pamoja na kuwa ni njia nzuri ya kuzuia ujauzito, vidonge vya
Uzazi wa Mpango vinatajwa kusababisha ugonjwa wa macho ujulikanao kama Glaucoma, unaoelezwa kuwa ni chanzo kikuu cha upofu.
Ugonjwa huu unaelezwa kuwa sababu kubwa ya kusababisha upofu kwa wanawake wanaotumia vidonge hivi kwa muda mrefu.
Hayo yamebainishwa kwenye Utafiti wa Afya na Lishe uliofanywa na Kituo cha Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa cha Marekani(CDCP).
Utafiti huo unasema kuwa, seli zilizoko katika neva za macho zina homoni za estrogen ambazo hufanya kazi ya kulinda macho, vidonge hivyo huingilia mchakato huo wa ulinzi kwa kupunguza kiwango cha homoni hizo.
Familia ya Waingereza, Kirstie Trup na Katie Gee, wote wenye
umri wa miaka 18, waliomwagiwa tindikali huko Zanzibar, wameiomba
Serikali ya Uingereza kuishinikiza Tanzania kuharakisha kuwawajibisha
waliohusika na tukio hilo.
Waingereza wa tindikali walia na serikali
Waingereza hao ambao walikuwa walimu wa kujitolea
katika shule ya St Monica, Tomondo, Zanzibar, walimwagiwa tindikali na
watu wawili wasiojulikana wakati walipokuwa kwenye matembezi ya jioni
katika eneo la Mji Mkongwe Agosti 7, mwaka huu.
Baada ya tukio hilo lililowajeruhi kiasi kikubwa
katika maeneo ya kifua na mikononi, walipewa matibabu katika hospitali
ya Aga Khan, Dar es Salaam, kisha wakarudishwa kwao kwa matibabu zaidi.
Alipowatembea wasichana hao hospitalini, Rais
Jakaya Kikwete alisema tukio hilo limetia aibu kwa mataifa ya nje na
kuliamuru Jeshi la Polisi kuhakikisha linawakamata na kuwafungulia
mashtaka wote waliohusika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni